IQNA

TEHRAN (IQNA) – Khitma ya siku ya saba ya marhum Ayatullah Mohammad Ali Taskhiri imefanyika Jumnne mjini Tehran.

Ayatullah Taskhiri, aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake Jumanne Agosti 18 2020 mjini Tehran akiwa na umri wa miaka 76. Mwanazuoni huo mtajika aliaga dunia hospitalini kutokana na matatizo ya moyo.

Ayatullah Taskhiri alikuwa mwanazuoni maarufu katika ulimwengu wa Kiislamu na aliwahi kuwa mkurugenzi wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu na halikadhalika mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ambapo alijitahidi sana kuilea umoja na mshikamano baina ya Waislamu duniani