IQNA

Msikiti Mkuu wa Sultan Qaboos

TEHRAN (IQNA)- Msikiti Mkuu wa Sultan Qaboos ulioko mjini Muscat ni msikiti mkubwa zaidi Oman na unaweza kubeba waumini 25,000. Msikiti huu una usanifu majengo wa kipekee na sasa mbali na kuwa eneo la ibada pia ni kivutio cha kitalii katika nchi hii ya Ghuba ya Uajemi.