Kongamano la 'Fikra za Nasrallah' lafanyika Tehran
IQNA - Maafisa wakuu wa Iran pamoja na wanazuoni na wanafikra kutoka nchi 13 wamehudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu Fikra za Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah, uliozinduliwa mjini Tehran Jumamosi, Novemba 9, 2024 kwa mnasaba wa Siku ya Arubaini tokea auawe shahidi kiongozi hiyo katika hujuma ya utawala wa kigaidi wa Israel.