Kisomo cha Mbinguni: Usomaji wa Qur’ani Tukufu wa qari Sheikh Al - Hadi Esfidani katika Ufunguzi wa Mashindano ya 41 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran
IQNA - Qari wa Iran, Sheikh Al - Hadi Esfidani, msomaji wa kimataifa wa Qur’ani Tukufu na mshindi wa kwanza wa mashindano ya 40 ya kimataifa ya Qur’ani nchini Iran, katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya 41 ya kimataifa ya Qur’ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyofanyika usiku wa leo, 27 Januari, katika mji wa Mashhad katika Ukumbi wa Quds wa kaburi takatifu la Imam Ridha (AS), alisoma aya za 9 hadi 12 za Surah Al-Isra na aya za mwanzo za Surah Al-Alaq.