IQNA

Waumini wanaoelekea Hija watembelea makaburi ya Baqi' huko Madina

IQNA – Makaburi ya Baqi' maarufu kama Janatul Baqi' katika mji mtakatifu wa Madina yamekuwa mahali takatifu na la kiroho kwa Waislamu, na mwaka huu, yamekuwa kivutio maalum kwa waumini kutoka mataifa mbalimbali ambao wanatembelea eneo hilo kabla ya kuelekea katika ibada ya Hija.

Ni mahali ambapo nyoyo za waumini huungana kwa kina na historia pamoja na hali ya kiroho, wakijihisi katika mazingira ya utulivu na dua. Baada ya ziara hii ya kiroho katika Baqi', waumini huaga kwa heshima na mapenzi Maimamu (A.S) waliolazwa hapo, huku nyoyo zao zikiwa nyepesi na zimejaa matumaini, kabla ya kuelekea Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija.

 
 
Kishikizo: janatul baqi