IQNA

Kiwanda cha 'Uswa' ni kiwanda kikubwa zaidi cha kuchapisha Qur'ani Tukufu nchini Iran na cha pili kwa ukubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Kiwanda hicho kilianzishwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya misahafu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maeneo mengine duniani.

Kiwanda cha Kuchapisha Qur'ani cha Uswa kilianzishwa kwa uwekezaji wa taasisi za wakfu nchini Iran na hivi sasa mbali na kuchapisha misahafu pia huchapisha vitabu vya kidini.