IQNA

Ali Shariati Mazinani maarufu kama Dakta Shariati, alizaliwa mwaka 1933 huko Kahak ( kijiji cha eneo la Mazinan katika mji wa Sabzevar, kaskazini magharibi mwa Iran) na alifariki Juni 18, 1977, mjini Southampton Uingereza.
Alikuwa msomi Mwirani aliyebobea katika taaluma za uandishi, sociolojia na utafiti wa kidini mbali na kuwa mwanamapinduzi, mwanaharakati wa kisiasa na mwananadharia wa Mapinduzi ya Kiislamu. Aliamini kuwa kurejea katika Uislamu halisi wa Kishia ni njia pekee ya kuleta uadilifu wa kijamii.
 
Dakta Shariati ni mashuhuri kwa jitihada zake za kuhuisha dini katika jamii na kuleta mwamko katika jamii ya Iran kuhusu namna utawala wa wakati huo wa Ufalme wa Pahlavi ulivyokuwa ukiwakandamiza wananchi.
 
Alifariki akiwa na umri wa miaka 44 nchini Uingereza na alizikwa karibu na Haram Takatifu ya Bibi Zaynab AS mjini Damascus Syria.  Picha hizi hapa chini ni za nyumba yake mjini Tehran ambayo sasa ni Jengo la Makumbusho.