IQNA

Jengo la kihistoria la Jumba la Makumbusho la Abgineh liko mjini Tehran na lilijengwa katika zama za watawala wa Qajar na lilikuwa makao ya waziri mkuu wa zama hizo kati ya mwaka 1921 hadi 1951. Mnamo 28 Juni 1998 jengo hilo lilisajiliwa kama athari ya kitaifa ya Iran. Jengo la Makumbusho la Abgineh ni jengo ambalo lina athari za kale za mada za kioo na seramiki.