IQNA

Kampeni ya Kimataifa ya Qur'ani ya “Fath”/ 21

Usomaji wa Tartili wa Aya ya 139 ya Surah Al-Imran kwa Sauti ya Ali Akbar Kazemi + Video

IQNA-Katika kuunga mkono kampeni ya Qur’ani Tukufu iitwayo Fath inayoendeshwa na Shirika la Habari la Kimataifa la Qur’ani (IQNA), msomaji mashuhuri na mwalimu wa kimataifa wa Qur’ani, Ali Akbar Kazemi, amesoma kwa tartili Aya ya 139 ya Surah Al-Imran.

Kazemi, ambaye pia ni jaji wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, alishiriki kwa bidii katika kampeni hii yenye lengo la kuhamasisha mapenzi na maarifa ya Qur’ani miongoni mwa Waislamu duniani.

Tizama video ya qiraa hapa chini

Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.
 

Kampeni mpya ya kimataifa ya Qurani kwa jina “Fath” imezinduliwa kwa lengo la kuinua morali ya majeshi ya Kiislamu na kueneza maadili ya Qurani ndani ya jamii, hasa kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Iran.

Kampeni hii, iliyoanzishwa na Shirika la Kimataifa la Habari za Qurani (IQNA), inahamasisha Waislamu kushiriki kwa kusoma aya maalum za Qurani Tukufu – ikiwemo Surah Al-Fath (aya 1–4), Surah An-Nasr, na aya ya 139 ya Surah Al-Imran.

Waandalizi wanasema usomaji huu unalenga kuwa nguvu ya kiroho kwa wapiganaji walioko mstari wa mbele, na pia kukuza ujumbe wa Qurani wa subira, msaada wa Mwenyezi Mungu, na ushindi wa haki juu ya batili.

Tuma usomaji wako kwa WhatsApp kupitia nambari: +989127397608

Kishikizo: Fath ، qurani tukufu