Qassemi alipata nafasi hiyo ya heshima baada ya kushinda nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani yaliyofanyika mwaka jana, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Waqfu na Masuala ya Misaada ya Iran.
Katika mashindano hayo ya 65 ya Kimataifa ya Usomaji na Kuhifadhi Qur’ani Tukufu (MTHQA), Qassemi alisoma aya za 11 hadi 21 za Surah Al-An'aam kwa ustadi mkubwa na sauti yenye taathira ya kiroho, akiwakilisha Iran mbele ya hadhira ya kimataifa.
Mashindano hayo yaliyoanza rasmi Jumamosi katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur, yanaendelea kutoka Agosti 2 hadi 9, yakibeba kaulimbiu ya mwaka huu: “Kuendeleza Jamii ya MADANI.” Jumla ya washiriki 71 kutoka nchi 49 wanashiriki katika tukio hili tukufu la kila mwaka.
Washindi wa mashindano haya watazawadiwa pesa taslimu: RM40,000 kwa mshindi wa kwanza, RM30,000 kwa wa pili, na RM20,000 kwa wa tatu, pamoja na mapambo ya thamani yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Kiislamu Malaysia (YAPEIM).
Katika toleo hili la mashindano, pia yupo mtaalamu mashuhuri wa Qur’ani kutoka Iran, Gholamreza Shahmiveh-Esfahani, ambaye anahudumu kama jaji katika baraza la waamuzi wa kimataifa.
Katika mashindano haya, kila Qari anaruhusiwa kufanya qiraa’ mara moja tu. Hatua ya awali ya mchujo ilifanyika kwa njia ya mtandao kupitia video.
Ifuatayo ni qiraa’ ya Mohsen Qassemi katika mashindano hayo:
4298122