IQNA

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema karibu Waislamu milioni moja katika eneo la Xinjiang nchini China, ambao aghalabu ni wa jamii za Uyghur na Kazakh wanashikiliwa katika kambi maalumu ambapo wanafunzwa itikadi za kikomunisti. Watoto wa Waislamu hao wa China nao wametenganishwa na wazazi wao na wamepelekwa shule maalumu za bweni.