IQNA

Ni miaka miwili tokea jeshi la Myanmar lishambulie mkoa wa Rakhine na kupelekea maelfu ya wakazi wa eneo hilo ambao ni Waislamu wa jamii ya Rohingya kukimbilia hifadhi katika nchi jirani ya Bangladesh. Bado mazingira ya wakimbizi hao kurejea katika ardhi zao za jaddi si nzuri na wanalazimika kuendelea kubakia katika kambi.