IQNA

TEHRAN (IQNA) - Takribani miezi minne iliyopita, serikali ya India iliondoa Hadhi Maalumu au mamlaka ya ndani ya eneo la Jammu na Kashmir. Hadhi hiyo maalumu ilikuwa ni kwa mujibu wa Kipengee cha 370 cha Katiba ya India.
Kabla ya kuchukuliwa uamuzi huo, serikali ya New Delhi ilituma maelfu ya askari katika eneo hilo linalozozaniwa sambamba na kuweka sheria kali ya kutotoka nje mbali na kufunga njia zote za mawasiliano ikiwemo intaneti na kuwatia mbaroni viongozi wengi wa Waislamu wa Kashmir.
Hatua hiyo ilivuruga uhusiano ambao ulikuwa tayari umeharibika na nchi jirani ya Pakistan ambayo katika kulalamikia kukandamiwza Wakashimiri, iliamua kushusha hadhi ya uhusiano wake wa kidiplomasia na India.