IQNA

Msikiti wa kwanza wenye kuzingatia utunzwaji mazingira (Eco-Friendly) umefunguliwa rasmi Disemba 5 katika mji wa Cambridge nchini Uingereza. Msikiti huo umefunguliwa katika sherehe ambayo imehudhuriwa na viongozi wa kidini na kisiasa kutoka kote katika ulimwengu wa Kiislamu na pia nchini Uingereza.