IQNA

Waislamu Uingereza

Idadi ya waliosilimu katika Msikiti wa Cambridge, Uingereza yafika 86 Mwaka Huu

18:13 - November 04, 2022
Habari ID: 3476033
TEHRAN (IQNA) - Kulingana na maafisa wa Msikiti wa Cambridge nchini Uingereza watu 86 wametamka shahada mbili (au tamko la imani ya Kiislamu) katika kituo hicho tangu Januari.

"Alhamdulillah, katika kipindi cha miezi kumi iliyopita watu 86 wamesilimu hapa #CambridgeCentralMosque," msikiti huo uliandika kwenye Twitter.  "Ikiwa imesalia miezi miwili kabla mwaka kuisha, tunakuomba utuombee dua tufike 100  Insha Allah!"

Kulingana na tovuti yake, viongozi hao wa misikiti wanafanya kazi pamoja na shirika dada la Cambridge Crescent kusaidia mtu yeyote ambaye ana nia ya  kuukumbatia Uislamu au tayari amesilimu.

Ripoti ya Kituo cha Utafiti cha Pew 2017 ilisema kuwa Uislamu ndio dini inayokua kwa kasi zaidi duniani..

Msikiti wa Cambridge ni msikiti wa kwanza wa kijani, yaani muundo wake umezingatia untunzaji mazingira, nchini Uingereza. Msikiti huo wa aina yake ulifunguliwa kwa mara ya kwanza kwa waumini mnamo Aprili 2019.

Msikiti umeundwa kuwa na mwanga wa kawaida usiotegemea umeme siku nzima na kuingiza hewa ya kutoka nje bila kutegemea viyoyozi, hata ukiwa umejaa kabisa, huku ukitumia mchanganyiko wa teknolojia ya kijani , ikijumuisha utekaji wa maji ya mvua, n.k  ili kupunguza kiwango chake cha uchafuzi wa hewa.

Msikiti huo, ambao unaweza kuchukua waumini 1,000, ni msikiti wa kwanza kujengwa kwa madhumuni huko Cambridge na umejitolea kwa ustawi wa kiroho na kijamii wa Waislamu wanaokadiriwa kuwa elfu sita wa jiji hilo.

Mnamo Novemba 2019, msikiti ulishinda tuzo ya kitaifa kwa muundo na mchango wake kwa jamii.

4096820

captcha