IQNA

Jalaludin Mohammad Balkhi Rumi, maarufu kwa lakabu ya Maulana, ni mmoja kati ya malenga mashuhuri zaidi Muirani wa karne ya tisa miladia.

Maulana alizaliwa katika mji wa Balkh na akiwa bado mtoto alienda katika mji wa Samarqand lakini baada ya muda mfupi aliondoka katika mji huo na kuelekea katika mji wa Konya nchini Uturuki.

Mashairi ya Maulana ni mashuhuri kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na kutumia mifano ya Qur'ani Tukufu. Kitabu chake cha Masnavi, au Masnavi-ye-Ma'navi ni athari yake iliyovuma sana.

Maulana aliugua homa kali na kuaga dunia mwaka 1273 Miladia akiwa na umri wa miaka 59 na alizikwa katika mji wa Konya.

Baada ya kifo chake, kaburi lake lilijengwa na msanifu majengo maarufu Tabrizli Badruddin kwa msaada wa kifedha wa mke wa Suleiman Parvaneh, Amiri wa Kiselujki na mwanae Maulavi. Kaburi hilo lenye usanifu majengo wa kipekee ni maarufu kama Kuba la Kijani na katika kuta zake kuna maandishi ya Bismillah na Ayatul Kursi kwa rangi ya samawati.