IQNA

Baada ya shughuli ya mazishi na kuusindikiza mwili mtoharifu wa Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wapiganaj jihadi wenzake katika miji ya Kadhimein, Karbala, Najaf nchini Iraq na kisha nchini Iran katika mji mtakatifu wa Mashhad na Tehran, jana tarehe 6 Januari miili hiyo ya mashahidi ilikuwa wageni katika Haram Takatifu ya Mwanamke Mkarimu wa Ahul Bayt AS, Bibi Maasouma SA mjini Qum.