IQNA

Msikiti wa Jamia ya Baiturrahman uko katikati ya mji wa Bande Aceh, katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia. Msikiti huu ni nembo ya dini, utamaduni, roho, nguvu, mapambano na utaifa wa Wasiamu wa Aceh pamoja na mapambano (muqawama) dhidi ya wakoloni Waholanzi. Msikiti huu uliweza kunusurika maafa makubwa ya tsunami ya Bahari ya Hindi mwaka 2004.