IQNA

Saudi Arabia siku ya Alhamisi Machi 5 iliweka vizingiti kwa ajili ya waumini wanaofika katika Msikiti Mtakatifu wa Makka kwa ajili ya kutufu katika Al Kaaba na mzunguko wa Sai baina ya Safa na Marwa. Maeneo hayo yatafungwa katika kipindi hiki ambapo Ibada ya Umrah imesitishwa kwa muda kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha Corona.