IQNA

Watu wa Ukanda wa Ghaza huko Palestina sawa na nchi zingine za Kiislamu wana mila na desturi maalumu za kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao mwaka huu umegubikwa na janga la corona. Ukanda wa Ghaza una matatizo mengi, kutokana na mzingiro uliowekwa na utawala wa Israel, na matatizo hayo huhisika zaidi katika Mwezi wa Ramadhani.