IQNA

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amezuru makaburi ya mashahidi wakuu watajika yaani Beheshti, Rajaei, Bahonar na mashahidi wa tukio la tarehe 7 mwezi Tir mwaka 1360 Hijria shamsiya na kumuomba Mwneyezi Mungu awainue waja wake hao.

Ayatullah Khamenei amezuru pia makaburi ya mashahidi mashuhuri na kuziombea roho takatifu za watetezi hao wa Uislamu na Iran. 

Ikumbukwe kuwa 12 Bahman mwaka 1357 Hijria Shamsia sawa na Februari Mosi 1979,  Imam Khomeini (MA) Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alirejea nchini na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka kadhaa. Mapokezi hayo makubwa ya wananchi wa Iran kwa Imam Khomeini hayajawahi kushuhudiwa mfano wake katika historia ya sasa ya dunia. 

Siku kumi baada ya kurejea nchini Imam,  yaani Februaria 11 1979, Mapinduzi ya Kiislamu yalipata ushindi kamili. Kipindi hicho cha siku kumi za baina ya kurejea Imam nchini hadi kupata ushindi kamili Mapinduzi ya Kiislamu, kinajulikana hapa nchini kama "Alfajiri Kumi". Kila mwaka hufanyika sherehe kubwa kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.