IQNA

Mwanakaligrafia wa Syria aandika Qur’ani akiwa nyumbani + Video

TEHRAN (IQNA)- Mwanakaligrafia wa Syria Muhammad Jalloul ambaye ameandika aya nyingi za Qur’ani sasa anafanya kazi zake akiwa nyumbani.

Akizungumza na kanali ya Al Jazeera, Jalloul anasema alianza kuandika kaligrafia ya Kiarabu akiwa na umri wa miaka 14 na alijifunza sanaa hii kwa mabungwa kama vile  Sheikh Mahmoud al Sabouni ambaye naye alikuwa mwanafunzi wa mwanakaligraifa maarufu wa Uturuki Hussein Hosni.

Jalloul amehusika katika kuandika mmoja kati ya Misahafu mikubwa zaidi duniani unaojulikana kama ‘Mushaf al Sham’. Ukubwa wa kila ukurasa wa Mushafu huo ni mita 2.1. Anasema aliandika Juzuu ya saba ya Mushafu huo na ilikuwa kazi ngumu sana.

Mwanakaligrafia huyo wa Syria ameshiriki katika mashindano ya kimataifa ya kuandika aya za Qur’ani Tukufu na alishinda zawadi yake ya kwanza mwaka 2003 katika mashindano yaliyoandaliwa na Benki ya Albaraka ya Uturuki. Aidha amepokea zawadi katika  mashindano yaliyofanyika katika miji ya Sharjah, Dubai na Istanbul katika mashindano tafauti. Mwaka 2011, Jalloul alishiriki katika mradi wa kaligrafia ya Qur’ani katika Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd. Aidha alishiriki katika mradi wa Msahafu wa Kitaifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu. Hivi sasa mwanakaligrafia huyu wa Uturuki anaishi katika mji wa Gaziantep Uturuki kutokana na matatizo ya usalama katika mji alikozaliwa wa Aleppo nchini Syria.

4004676