IQNA

Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr mwanazuoni aliyeleta mwamko wa Kiislamu + Video

TEHRAN (IQNA)- Klipu ifuatayo inaangazia kwa kifupi maisha na nyakati za mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Shahidi Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr.

Alizaliwa Machi 1, 1935 katika eneo la Al Kadhimya katika mkuu wa Iraq, Baghdad. Baba yake, Haydar al-Sadr alikuwa mwanazuoni aliyeheshimika na babu yake. Ayatullahil Udhma Ismail al-Sadr naye pia alikuwa Marjaa Taqlid katika zama zake.

Muhammad Baqir al-Sadr alimpoteza baba yake akiwa na umri wa miaka mitatu  na hapo kaka yake, Sayyed Esmail akawa mlezi wake. Akiwa mtoto Sadr alijifunza Qur'ani Tukufu na elimu nyingine za kidini na akafikia daraja ya ijtihad akiwa kijana.

Amina Sadr, ambaye pia ni Bint-al-Huda, alijifunza dini kutoka kwa ndugu yake,, Muhammad Baqir.

Alihamia Najaf mwaka 1945, akiwa na familkia yake na hapo akaanza rasmi masomo ya kidini. Alihudhuria darsa za fiqhi za Ayatullahil Udhma Sayyid Abu al-Qasim al-Musawi al-Khoei na Ayatullah Sheikh Muhammad Ridha al-Yasin.

Alikuwa mmoja wa walimu wakubwa wa chuo cha kidini mjini Najaf Iraq kiasi kwamba, nadharia zake katika elimu ya Usulu Fiqhi zilipewa umuhimu mkubwa na wasomi wengine wa Kiislamu. Msomi huyu aliyekuwa na uelewa na uwezo wa hali ya juu wa kielimu, aliuarifisha Uislamu kwa njia sahihi. Kwa kipindi kifupi Ayatullah Sadr aligeuka na kuwa kiongozi wa kifikra na kisiasa wa wananchi wa Iraq na kuyapa mwelekeo mpya mapambano ya wananchi wa Iraq. Aidha alikuwa mtetezi wa harakati za Umoja wa wa Kiislamu. Baada ya muda fulani utawala wa nchi hiyo ambao ulihisi hatari kutokana na harakati za Ayatullahi Sadr ulimtia mbaroni na kisha kumuua shahidi mwanazuoni huyo mashuhuri pamoja na dada yake, licha ya malalamiko makubwa ya maulama na wananchi Waislamu wa Iraq. Miongoni mwa vitabu vya msomi huyo ni pamoja na kitabu kiitwacho "Hamasa ya Nuru", "Falsafa Yetu", "Mwanadamu wa Leo na Matatizo ya Kijamii", na "Ukhalifa wa Mwanadamu na Ushuhuda wa Mitume."

Taqribani miaka 41 iliyopita utawala wa Baathi nchini Iraq uliwaua Shahidi Sayyid Muhammad Baqir-Sadr na dada yake Bintul Huda.

4007737