iqna

IQNA

iraq
Sala ya Idu
IQNA - Sala ya Idul Fitr katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq ilishuhudia mahudhurio makubwa ya waumini na wafanyaziyara siku ya Jumatano.
Habari ID: 3478671    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/11

Mashindano ya Qur'ani
IQNA – Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala hivi karibuni ilihitimisha awamu ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yajulikanayo kama Tuzo ya Kimataifa ya Al-Ameed ya Kusoma Qur’ani, ambayo yamefanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3478612    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/01

Mapambano ya Kiislamu yaani Muqawama
IQNA - Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (muqawama) ya al-Nujaba ya Iraq amesema harakati hiyo itaendelea kulenga ngome za utawala wa Kizayuni kwa lengo la kuonyesha mshikamano na Palestina.
Habari ID: 3478414    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/26

Ugaidi wa Marekani
IQNA-Utawala wa Marekani unaendelea kulaaniwa kufuatia hujuma yake ya kigaidi iliyopelekea kuuawa shahidi Abu Baqer al-Saadi, mmoja wa makamanda wa muqawama wa Kiislamu nchini Iraq.
Habari ID: 3478325    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/09

Siasa
IQNA-Serikali ya Iraq imelaani vikali mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Marekani dhidi ya maeneo kadhaa ya nchi hiyo na nchi jirani yake Syria na kusisitiza kuwa, hujuma hizo zimekiuka mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo.
Habari ID: 3478297    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/03

Mashindano ya Qur'ani
IQNA – Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS) katika mji wa Karbala nchini Iraq imetangaza tukio lake kubwa la Qur'ani, "Tuzo ya Kimataifa ya Al-Ameed ya Kuhifadhi Qur'ani," ambayo itafanyika kama mashindano ya televisheni yaliyo wazi kwa wasomaji kutoka nchi zote.
Habari ID: 3478296    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/03

IQNA - Siku ya 27 ya mwezi wa Hijri wa Rajab iliteuliwa kuwa Siku ya Kitaifa ya Kurani Tukufu nchini Iraq.
Habari ID: 3478283    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/01

Siasa
IQNA - Kutumia neno "Israel" katika kuashiria utawala wa Tel Aviv kumepigwa marufuku katika vyombo vya habari vya Iraq, afisa mmoja alisema.
Habari ID: 3478213    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/18

Vita dhidi ya ugaidi
IQNA-Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa, limevurumisha makombora ya balestiki kulenga ngome za magaidi wa Syria, waliohusika katika mashambulizi ya hivi karibuni nchini Iran, pamoja na kituo cha ujasusi cha Israel katika eneo la Kurdistan ya Iraq.
Habari ID: 3478201    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/16

Muqawama
IQNA - Makamanda wa harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis walikuwa wapiganaji wakubwa waliopata ushindi dhidi ya ugaidi wa kimataifa.
Habari ID: 3478166    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/08

Qur'ani Tukufu
IQNA – Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) inapanga kuandaa mashindano ya kila mwaka ya kusoma Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3478064    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/20

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
BAGHDAD (IQNA) - Washiriki katika mkutano wa kutetea Qur'ani Tukufu nchini Iraq wamesisitiza haja ya kutunga sheria za kimataifa zinazoharamisha kuvunjiwa heshima matakatifu ya kidini.
Habari ID: 3477350    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/28

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
BAGHDAD (IQNA)- Wananchi wa Iraq waliokuwa na ghadhabu wameuvamia ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad na kuchoma moto sehemu moja ya ofisi za ubalozi huo, kulalamikia kibali cha pili kilichotolewa na serikali ya Stockholm cha kuruhusu kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Habari ID: 3477309    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/20

Harakati za Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Maonesho ya Qur’ani Tukufu yamezinduliwa katika Chuo Kikuu cha Alkafeel katika mji mtakatifu wa Najaf, Iraq.
Habari ID: 3476632    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/27

TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa Mfawidhi wa Haram Takatifu za Al-Kadhimayn nchini Iraq, zaidi ya wafanyaziyara milioni 12 walitembelea eneo hilo takatifu alikozikwa Imam Kadhim (AS). Mjumuiko huo umefanyika kwa mnasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi mtukufu huyo.
Habari ID: 3476577    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/17

Harakati ya Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Taasisi za Qur'ani nchini Iraq zinashinikiza nchi hiyo kuitaja siku moja katika kalenda kuwa 'Siku ya Qur'ani Tukufu.'
Habari ID: 3476529    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/07

Jinai za Marekani
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia' al-Sudani amemuenzi kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwenzake wa Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad miaka mitatu iliyopita, na kusema kuwa mauaji hayi yalikuwa "shambulio kali" dhidi ya uhuru na mamlaka ya kujitawala Iraq.
Habari ID: 3476365    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/06

Maonyesho ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq utakuwa mwenyeji wa awamu ya pili ya Maonyesho ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu ndani ya wiki chache kuanzia sasa.
Habari ID: 3476364    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/06

Uislamu na Ukristo
TEHRAN (IQNA) – Katika mnasaba wa Krismasi, ambayo ni siku ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa Nabii Isa Masih bin Maryam-Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake-,, qari wa Iraq alisoma aya za Sura Al Imran ya Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3476322    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/28

Uislamu na Ukristo
TEHRAN (IQNA) – Papa Francis, katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, alisafiri hadi Iraq mwezi Machi mwaka jana.
Habari ID: 3476271    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/19