"Sheikh Muhammad al Laythi alifariki miaka mitano mapema kabla ya baba yake. Wakati baba yake alipofariki, kaburi alimokuwa Laythi lilifunguliwa ili baba yake azikwe," anasimulia Sheikh Tarouti.
Anaendelea kusema kuwa: "Mhusika katika masuala ya makaburi akiwa mle ndani akiwa na hali ya mshangano alimuita mmoja ya marafikizi Laythi na kumuambia, 'njoo umtizame rafiki yako."
Walitizama vidole vyake vilkuwa vimenyooka na mikono ilikuwa haina mabadiliko yoyote na mwili wake pia walipougusa walihisi hauna mabadiliko yoyote na umebakia salama."
Sheikh Muhammad Muhammad al-Laythi alizaliwa mwaka 1949 katika familia ya wasomaji na wanaohifadhi Qur'ani katika mkoa wa Ash Sharqia ambapo alijifunza Qur'ani akiwa yungali mtoto.
Alijifunza qiraa ya Qur;ani kutoka kwa baba yake na maustadhi wengine katika mkoa huo na kisha akajiunga na Radio ya Qur'ani ya Misri kama qarii mwaka 1984. Aliwahi kushiriki katika vikao vya kusoma Qur'ani katika nchi nyingi duniani kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, India, Pakistan, Ujerumani na Afrika Kusini. Aliaga dunia Machi 5 2006.