iqna

IQNA

IQNA – Shule ya Qur'ani ya Novi Pazar nchini Serbia ni miongoni mwa vituo muhimu zaidi vya elimu ya Qur'ani katika eneo la Balkan, ikijitahidi kufufua utambulisho wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu wa eneo hilo na kuwafundisha Qur'ani Tukufu pamoja na tafsiri yake kwa wenye nia.
Habari ID: 3481029    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/02

IQNA – Washindi wa upande wa wanaume katika awamu ya kimkoa ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran, yaliyofanyika Tehran, wametangazwa rasmi katika hafla ya kufunga mashindano hayo na kukabidhiwa vyeti vya heshima pamoja na zawadi za fedha.
Habari ID: 3481028    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/01

IQNA – Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar inaendesha darasa maalum la kiangazi la Qur’ani Tukufu kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kuhifadhi na kusoma Qur’ani miongoni mwa wanafunzi.
Habari ID: 3481027    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/01

IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Kiislamu kutoka Nigeria amezindua mradi wa kipekee wa tarjuma ya Qur’ani Tukufu kwa lengo la kuwafikishia ujumbe wa Allah kwa jamii zinazozungumza Kiyoruba duniani kote.
Habari ID: 3481025    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/01

IQNA – Mwanaume mwenye umri wa miaka 27 nchini Ufaransa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kitendo cha kuvunjia heshima Qur'ani, Kitabu Kitakatifu cha Uislamu.
Habari ID: 3481024    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/01

IQNA – Kundi la walimu na maqarii mashuhuri wa Qur’ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeandika barua ya wazi kwa maqari wa Misri, likiwataka wachukue msimamo dhabiti dhidi ya ukatili wa utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusimama pamoja na watu wanyonge wa eneo hilo.
Habari ID: 3481022    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/30

IQNA – Afisa mmoja kutoka Wizara ya Elimu ya Iran amesema kuwa shule 1,200 za kuhifadhi Qur’ani zinapangwa kuzinduliwa nchini ili kusaidia mpango wa kuwafundisha wahifadhi milioni 10 wa Qur’ani.
Habari ID: 3481018    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/30

IQNA-Kozi ya kiangazi ya wanawake ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika Msikiti Mtukufu wa Masjid al-Haram, Makkah, imekamilika kwa mafanikio, ambapo washiriki zaidi ya 1,600 wametimiza masharti ya programu hiyo.
Habari ID: 3481013    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/28

IQNA-Mji wa Al Hoceima, ulioko kaskazini mwa Morocco, umeandaa tamasha lake la kwanza la Qur’ani Tukufu, likiwatambua washiriki mashuhuri wa mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani. Tukio hilo lilianza Ijumaa, Julai 25, na liliambatana na maadhimisho ya miaka 26 tangu Mfalme Mohammed VI achukue madaraka ya kifalme.
Habari ID: 3481012    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/28

IQNA- Mahdi Ghorbanali, qari wa swala ya Ijumaa mjini Tehran, amejiunga na kampeni ya Qur’ani ya IQNA iitwayo “Fath” kwa kusoma aya ya 139 ya Surah Al-Imran.
Habari ID: 3481008    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/27

IQNA – Jumamosi, tarehe 26 Julai 2025, ulimwengu wa Kiislamu uliadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Sheikh Muhammad Abdul Wahhab Al-Tantawi, gwiji wa usomaji wa Qur’ani katika enzi ya dhahabu ya Misri.
Habari ID: 3481006    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/27

IQNA – Chuo cha Kisayansi cha Qur’ani kinachohudumu chini ya Utawala wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS) kimeandaa mfululizo wa vikao vya Qur’ani Tukufu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Babylon nchini Iraq, kwa mnasaba wa mwezi wa Muharram.
Habari ID: 3481001    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26

IQNA – Mwanamke mkongwe kutoka Aswan, Misri, aliyekuwa hajui kusoma wala kuandika kwa muda mrefu, hatimaye ameweza kutimiza ndoto yake ya kusoma Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 76.
Habari ID: 3481000    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26

IQNA – Kwa lengo la kueneza mafundisho ya Uislamu, maafisa wa serikali ya Morocco wamegawa nakala za Qur’ani Tukufu kwa Wamorocco wanaoishi nje ya nchi waliporejea nyumbani.
Habari ID: 3480999    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/26

IQNA – Wanafunzi thelathini wa Qatar wameshiriki katika kozi ya majira ya joto ya wiki tatu iliyoandaliwa na Kituo cha Elimu ya Qur'ani cha Al Noor kwa lengo la kuboresha kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kukuza ujuzi wa kielimu.
Habari ID: 3480998    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/25

IQNA – Shughuli za Msafara wa Qur'ani wa Arbaeen wa Iran mwaka huu nchini Iraq zinatarajiwa kuanza tarehe 5 Agosti, kwa mujibu wa afisa mmoja.
Habari ID: 3480995    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/25

Kampeni ya Kimataifa ya Qur'ani ya “Fath”/ 21
IQNA-Katika kuunga mkono kampeni ya Qur’ani Tukufu iitwayo Fath inayoendeshwa na Shirika la Habari la Kimataifa la Qur’ani (IQNA), msomaji mashuhuri na mwalimu wa kimataifa wa Qur’ani, Ali Akbar Kazemi, amesoma kwa tartili Aya ya 139 ya Surah Al-Imran.
Habari ID: 3480993    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/24

IQNA – Warsha ya mafunzo kuhusu misingi ya Qira’at kumi za Qur’ani Tukufu imezinduliwa katika Msikiti wa Mtume (SAW) - Al Masjid an Nabawi, mjini Madina, Saudi Arabia.
Habari ID: 3480987    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/23

IQNA – Afisa mmoja wa utamaduni nchini Iran ameeleza kuwa matembezi ya Arbaeen ni dhihirisho la wazi la mafundisho ya Qur’ani Tukufu kwa vitendo.
Habari ID: 3480985    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/23

IQNA – Mkutano wa 20 wa wataalamu wa Qur’ani, makari na wahifadhi wa Iran utafanyika mwezi Novemba mwaka huu chini ya usimamizi wa Baraza Kuu la Qur’ani.
Habari ID: 3480976    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/21