IQNA

TEHRAN (IQNA) - Masjid Istiqbal ni msikiti mkubwa zaidi Kusini Mashariki mwa Asia na uko katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta. Msikiti huo una uwezo wa kubeba waumini 120,000 wakati moja.

Msikiti huo ulifunguliwa mwaka 1978 baada ya ujenzi uliodumu kwa muda wa miaka 17. Msikiti huo ulizinduliwa katika sherehe uhuru wa nchi hiyo kutoka mkoloni Mholanzi.