IQNA

Msafara wa mazishi wa mwandishi habari Shireen Abu Akleh

TEHRAN (IQNA)- Msafara wa mazishi ya mwandishi habari Mpalestina Shireen Abu Akleh, ulisahmbuliwa na askari wa utawala wa Kizayui wa Israel Ijumaa katika mji wa Quds (Jerusalem) Mashariki unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Mapema Jumatano, mwandishi wa habari ya televisheni ya al Jazeera, Shireen Abu Akleh, 51, alipigwa risasi na kuuliwa shahidi kikatili na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati akiwa kwenye kazi yake ya kuripoti uvamizi wa kijeshi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin.

 
 
Kishikizo: abu akleh