IQNA

Maktaba yenye muundo wa kitabu mjini Dubai

TEHRAN (IQNA)- Maktaba ya Umma ya Muhammad bin Rashid imefunguliwa wiki iliyopita huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu
Makataba hiyo ina muunda wa rehl ambayo ni chombo cha mbao ambacho hutumika kuwekelea msahafu unaopusoma na hivyo kufanya jengo hilo kuonekana lenye usanifu majengo wenye muundo wa kitabu.

Maktaba hiyo imegharimu dola milioni 272 kuijenga na ina ghorofa saba na maktaba tisa za kitaalamu zenye vitabu zaidi ya milioni moja vikiwemo vitabu vya kidijitali.