IQNA

Tetemeko la ardhi Afghansitan ni mtihani kwa madai ya Wamagharibi

TEHRAN (IQNA)- Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 kwenye kipimo cha rishta ulitikisha eneo la mashariki mwa Afghanistan siku chache zilizocpita ambapo watu zaidi ya elfu moja walipoteza maisha na wengine karibu 1,500 wamejeruhiwa.

Wakati huo huo kutokana na vikwazo vya madola ya Magharibi hasa Marekani dhidi ya Afghansitan baada ya utawala wa Taliban kuchukua hatami za uongozi nchi hiyo imeshindwa kupata fedha zake zilizo katika mabenki ya madola ya Magharibi. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanataka fedha hizo ziachiliwe na nchi hiyo masikini ipewe misaada kukabiliana na janga hilo. Nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu bado zinaendelea kushikilia fedha za Afghanistan katika wakati huu mgumu.