IQNA

Souq Waqif: Msongamano katika Soko la Jadi la Qatar

TEHRAN (IQNA) – Soko la kitamaduni lenye historia ya miaka 250, Souq Waqif liko katikati mwa Doha na sasa linakaribisha maelfu ya watalii wa kigeni ambao wamekuja Qatar kutazama Kombe la Dunia la FIFA la 2022.

Kati ya bidhaa zinazouzwa katika soko hilo ni nguo za kitamaduni, viungo, kazi za mikono, na zawadi huku pia kuwa nyumbani kwa mikahawa kadhaa. Soko hilo lilikarabatiwa mnamo 2006.