Kitovu chake kilikuwa ni katika mji wa Gaziantep wa Uturuki ambapo mamia ya majengo yameporomoka.Masaa machache baadaye kulijiri mtetemeko mwingine wa ardhi uliokuwa na ukubwa 7.6 kwenye kipimo cha rishta. Picha hizi zinaonyesha hali baada ya mitetemeko hiyo ambayo imepelekea maelfu ya watu kupoteza maisha na uharibifu mkubwa.