IQNA

Qur'ani Tukufu

Msikilize Ustadh Yusuf Al-Bahtimi akisoma Qur'ani Tukufu

TEHRAN (IQNA)- Marhum Kamel Yusuf Al-Bahtimi, alikuwa msomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu nchini Misri. Katika klipu hii anasikika akisoma aya za Sura An Naml aya za 29-31 zisemazo:

(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu. Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri.

Hamad Zaki Yusuf, anayejulikana kama Kamel Yusuf Al-Bahtimi katika kijiji cha Bahtim mkoa wa Qalubiyeh, alikuwa msomaji bora wa Kimisri wa Qur'ani ambaye alipata umaarufu wa ajabu katika miaka ya 1950 hadi 1960. Aliaga dunia mnamo Juni 12, 1348.

Kishikizo: qurani tukufu ، kamel yusuf