Vita vya miaka 8 vya Iraq dhidi ya Iran (1980-1988) vinajulikana kama "Kujihami Kutakatifu" nchini Iran.
Mji huo wa sinema uko Shahr-e Rey, kilomita 25 kutoka barabara kuu ya Tehran-Qom, kwenye eneo la ardhi la zaidi ya hekta 550.
Mchanganyiko huo unajumuisha maeneo mbalimbali kama vile ziwa, vituo vya kijeshi vya Iraq, mashamba n.k.
Eneo hilo limekuwa eneo la kuzalisha aina tofauti za sinema za Iran. Filamu nyingi mashuhuri katika nyanja za "Kujihami Kutakatifu" na mada za kidini zimetengenezwa hapa.
Filamu nyingi zinazohusiana na vita zimetengenezwa na halikadhalika filamu za kidini kama ili Silsila ya vipindi vya Nabi Yusuf (AS).
Katika nchi nyingi zilizo na tasnia yenye nguvu ya sinema, majengo ya sinema ni sehemu muhimu ya makumbusho ya sinema hai. Sio tu kuwa waandaaji wa filamu lakini pia husaidia kupata mapato kwa tasnia ya sinema wakati maeneo hayo yanapokodishwa.
Kutembea katika eneo hili kunaibua taswira ya ushujaa wa wanaume na wanawake ambao walisimama dhidi ya utawala wa Baath wakati wa vita hivyo vya kulazimishwa. Wakati wa vita hivyo wapiganaji shujaa wa Iran walihakikkisha hakuna hata inchi moja ya ardhi yao iliyototekwa na adui.