IQNA

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Wiki ya Kijihami Kutakatifu yaadhimishwa Iran

22:59 - September 22, 2022
Habari ID: 3475825
TEHRAN (IQNA)- Leo Alkhamisi tarehe 25 Safar 1444 Hijria sawa na 22 Septemba 2022 inayosadifiana na 31 Shahrivar 1431 Hijria Shamsiya inaadhimishwa kama kama mwanzo wa 'Wiki ya Kujihami Kutakatifu'

Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita, majeshi ya dikteta wa zamani wa Iraq Saddam Hussein yalianza kufanya mashambulio makubwa ya anga na nchi kavu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hivyo vita vya miaka minane vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran vikawa vimeanza. Jeshi la Iraq lilikuwa limefanya uvamizi na mashambulizi kadhaa katika maeneo ya mpakani ya Iran miezi kadhaa nyuma. Magari ya deraya na vikosi 12 vya jeshi la nchi kavu la Iraq viliyashambulia maeneo ya mipaka ya kusini magharibi mwa Iran. Mapambano makali ya wananchi wa Iran yaliwalazimisha askari wa Saddam kurejea nyuma hadi kwenye mipaka inayotambulika kimataifa. Oparesheni za Iran za kukabiliana na uvamizi huo wa Saddam ni maarufu kama "Kujihami Kutakatifu".

Mjini Tehran maadhimisho haya yanafanyika jirani na haram ya Imam Ruhullah Khomeini (MA) mwasisi na mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo viongozi wa serikali na makamanda mbalimbali wa ngazi za juu wa jeshi wameshiriki katika maadhimisho haya muhimu katika historia ya Iran.

Maadhimisho ya 'Wiki ya Kujihami Kutakatifu' yameanza kwa mbwembwe za aina yake, ambapo mapema leo asubuhi vikosi tofauti vya Jeshi laAkizungumza katika gwaride ambalo limefanyika mjini Tehran, Mkuu wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Meja Jenerali Mohammad Baqeri, amesema: "Kujihami kutakatifu kulionyesha ustahiki na fadhila za taifa la Iran ambalo pamoja na kuwepo hujuma ya maadui waliokuwa wakipata himaya ya uistikbari wa kimataifa, taifa la Iran liliweza kusimama kidete." Iran vimepiga magwaride hapa jijini Tehran na katika miji mingine ya Iran

Ikiwa ni katika mkesha wa maadhimisho ya Wiki ya Kujihami Kutakatifu, maveterani wa vita, makamanda na wapiganaji wa vita vya kujitetea kutakatifu na familia za mashahidi walikutana siku ya Jumatano asubuhi na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ukumbi wa Husseiniyah ya Imam Khomeini (MA).

Katika maadhimisho hayo, Ayatullah Khamene alisema kwamba vita hivyo vilisababishwa na sera za kistratijia za mabeberu za kuchochea uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran na kuongeza: Licha ya ungaji mkono mkubwa na wa pande zote wa mataifa yenye nguvu duniani kwa Saddam mwenye tamaa na uchu wa madaraka, lakini vita hivyo viligeuka kutoka kuwa tishio la uhakika na kubwa na kuwa fursa kubwa kwa msingi wa vipengele vitatu vya "nguvu ya kihamasa ya mapinduzi, uongozi athirifu wa Imam na sifa za kipekee za taifa shupavu la Iran". Ufafanuzi sahihi na wa kina wa kipindi hicho cha hamasa na cha kusisimua cha historia ya Iran bila shaka utakidhaminia kizazi kipya cha vijana wetu kudumishwa mafanikio ya mapinduzi.

3480584

 

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha