Sherehe katika Haram ya Imam Ali (AS) katika siku ya kukumbuka kuzaliwa kwake
IQNA- Hali ya furaha imejaa katika Haram au kaburi takatifu la Imam Ali (AS) huko Najaf, Iraq katika siku ya leo, 13 Rajab, ambayo ni siku ya kukumbuka kuzaliwa mtukufu huyo ambaye ni Imamu wa Kwanza wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Hali katika kaburi hilo imejaa waumini wakifanya ibada, huku wafanyaziara na wageni wakikusanyika pamoja kutoa heshima zao na kushiriki katika hafla mbalimbali za kidini.