IQNA

Maonyesho ya kaligrafia kuhusu Imamu Hussein (AS) Yafunguliwa Mashhad

IQNA – Maonyesho ya sanaa ya kaligrafia yaliyopewa jina la "Machozi ya Waridi", yamezinduliwa kwa mnasaba siku za maombolezo za siku kumi za mwanzo za Mwezi wa Muharram, yakionyesha kazi za mtaalamu mahiri wa hati za kaligrafia, Ali Akbar Rezvani.

Maonyesho haya pia yanajumuisha kazi za  Masoumeh Mohammadiya pamoja na Fatemeh Rezvani. Yameandaliwa na Taasisi ya Ubunifu wa Kisanaa katika Shirika la Astan Quds Razavi, na yataendelea kwa muda wa siku tano kuanzia Jumamosi, Juni 28, 2025, katika Nyumba ya Sanaa ya Rezvan jijini Mashhad.

.