IQNA

Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu Akagua Huduma Zinazotolewa kwa Mahujaji wa Arbaeen

IQNA – Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija na Ziyara, pamoja na maafisa wengine kadhaa wa Kiirani walioko Karbala, Iraq, wamekagua huduma zinazotolewa kwa wafanyaziyara wa Arbaeen.

Hujjat-ul-Islam Seyed Abdol Fattah Navab, akiwa pamoja na mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara la Iran, walifanya ziara za kina za uwanjani kwa lengo la kutathmini kwa karibu huduma za kiutamaduni, kijamii na kimatibabu zinazotolewa kwa wafanyaziyara.

Walifanya vikao na maafisa wa Mawjuva (vituo vya huduma kwa wafanyaziyarai), vituo vya matibabu, na makao makuu ya Hilali Nyekundu mjini Karbala, wakakutana na mlezi wa haram tukufu ya Bwana wetu Hazrat Abbas (AS), na pia wakatembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji huo mtukufu.