IQNA – Hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya Sanaa za Qur’an ya Duha, yaliyoandaliwa na Shirika la Qur’an la Wasomi wa Iran, ilifanyika jioni ya Jumapili, Novemba 16, 2025, katika Makumbusho ya Sanaa za Kidini ya Imam Ali (AS), mjini Tehran.
Maonesho hayo yameandaliwa chini ya kaulimbiu ya kuamsha matumaini na kuhimiza tafakuri juu ya Surah Ad-Duha katika Qur’an Tukufu.