TEHRAN (IQNA)-Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika Ijumaa 14 Aprili katika kila pembe ya Iran ya Kiislamu kwa kauli mbiu kuu "Palestina mhimili wa umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu; Quds inakaribia kukombolewa".
Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa ubunifu wa Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.