Ukiwa unajulikana kam 'mlima cha rehema,' Mlima Arafat ni eneo la khutba ya Kuaga ya Mtume Muhammad (SAW), iliyotolewa miaka 1,435 iliyopita, ambapo alizungumzia usawa na umoja kati ya Waislamu.
Safari ya kuelekea mlima huo ulioko kilomita 20 kusini mashariki mwa Makka, ilianza mapema kabla ya mapambazuko, huku mahujaji wakitembelea umbali huo kwa miguu. Hisia zilienea sana miongoni mwa waumini huku wakiinua mikono yao katika dua, wengi wakibubujikwa na machozi, wakitafuta rehema, Baraka za Mwenyezi Mungu..