Picha: Kikao cha Usomaji wa Qur'an Katika Haram ya Shah Cheragh, Shiraz
IQNA – Haram tukufu ya Shah Cheragh (AS) iliyoko katika jiji la Shiraz, kusini mwa Iran, iliandaa kikao cha usomaji wa Qur'an Tukufu jioni ya Jumatatu, tarehe 14 Julai 2025.
Katika kikao hiki kilichojaa nuru na utulivu wa kiroho, maqari maarufu Mohammad Reza Pourzargari na Mohammad Saeed Masoumi walisoma aya tukufu kutoka katika Kitabu Kitakatifu cha Allah, kwa sauti za kuvutia na zenye khushuu.