IQNA

Maonyesho yenye anuani ya 'Mpweke zaidi ya Masihi' yameandaliwa kwa munasaba wa siku hizi za Arobaini ya Imam Hussein AS na mada kuu ni masaibu ya Ahul Bayt wa Mtume SAW katika tuko la Ashura.

Maonyesho hayo ambayo yameanza mjini Tehran katika Bustani ya Wilayat yanatazamiwa kuendelea hadi Novemba 8. Katika maonyesho hayo kuna zaidi zaidi ya kazi 400 za sanaa na pia kuna wasanii. Wasimamizi wanasema kila usiku kuna wageni takribani 7000 wanaotembelea maonyesho hayo.