IQNA

Wapalestina waandamana Wazayuni kupora maeneo zaidi ya Ukingo wa Magharibi

Makumi ya Wapalestina wanaoishi katika mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wameandamana kupinga mpango wa utawala wa Kizayuni ambao unalenga kuteka ardhi zaidi za Wapalestina katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa, Wapalestina waliokuwa na hasira pamoja na viongozi kadhaa wa makundi ya Kipalestina siku ya Jumatatu walishiriki katika maandamano makubwa katika maeneo kama vile Al Khalil, Tulkaram na Tubasi na kubainisha upinzani wao kwa mpango wa utawala wa Kizayuni wa kukalia kwa mabavu eneo la Ukingo wa Magharibi. Maandamano hayo yamefanyika kwa mnasaba wa mwak wa 53 wa Naksa au siku ambayo Wapalestina walipata pigo. Washiriki walitoa nara kama vile 'Tunapinga kupora ardhi' , 'Ardhi ni ya taifa letu, na 'Tutakufa ili Palestina iwe Hai'.