IQNA

TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wa Utawala wa Kizayuni wa Israel wamwashambulia na kuwafyatulia risasi Wapalestina ambao walikuwa wanashiriki katika mazishi ya Mpalestina, Ibrahim Mustafa Abu Yakub.

Shahidi Abu Yakub aliuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi iliyotekelezwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel. Mazishi ya mwendazake yalifanyika katika kijiji cha Salfit, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Washiriki katika mazishi walikuwa wamebeba bendera za Palestina huku wakitamka nara ya Allahu Akbar.