TEHRAN (IQNA) - Mamia ya Wapalestina wameandamana katika Ukanda wa Ghaza kulaani hatua ya mahakama ya utawala haramu wa Israel kufunga lango la Bab al-Rahma la Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).
Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yaliyokuwa na maandishi kama vile " Tutalinda Quds Kwa Damu Zetu", "Mshikamano na Watu wa Quds', na 'Tunaunga Mkono Bab al Rahma"