IQNA

TEHRAN (IQNA)- Waombolezaji, aghalabu wakiwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia, kutoka Iraq na mataifa mengine duniani wakiwa katika matembezi ya kuelekea Karbala kwa ajili ya kumbukumbu ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Maadhimisho siku ya Arubaini (Arobaini au Arbaeen) hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala mwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.