IQNA – Ukiendelea na mnyororo wake wa kimfumo wa kuzuia uhuru wa maoni na kukandamiza wataalamu na watendaji wa kiraia, ufalme wa kiimla wa Bahrain umemkamata mtafifi mwelekeo wa Shia.
Habari ID: 3482408 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/27
IQNA-Waislamu wa mji wa Witu katika Kaunti ya Lamu, pwani ya Kenya wameshiriki katika maombolezo ya siku ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali (AS), watu wa nyumba yake na wafuasi wake watiifu katika uwanda wa Karbala, Iraq mwaka 61 Hijria Qamaria. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Umul Banin mjini humo. Hizi hapa chini klipu za maombolezo hayo.
Habari ID: 3482406 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Haram takatifu ya Imam Hussein (AS) katika mji wa Karbala nchini Iraq ilijaa mazuwaru usiku wa kuamkia Ashura, ambao uliangukia usiku wa Alhamisi katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3482405 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Maelfu ya Waislamu wa Kishia na wapenzi wa Ahlul-Bayt (AS) katika miji mbalimbali ya Ulaya waliinua bendera za maombolezo ya Muharram na kupaza mwito wa “Labayka Ya Hussein”.
Habari ID: 3482404 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Hafla ya maombolezo ya Ashura iliandaliwa siku ya Ijumaa kwenye kaburi la shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa harakati ya mapambano ya Hizbullah ya Lebanon.
Habari ID: 3482403 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/26
IQNA – Mwamko wa Imam Hussein (AS) haukuwa uasi wa kimageuzi uliotokea na kuishia katika kurasa za historia; bali ulikuwa ni mkondo wa kifikra wenye malengo matukufu na maadili ya kimalakuti yanayovuka mipaka ya zama.
Habari ID: 3482401 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/25
IQNA-Wairani katika mji mkuu Tehran, majiji, miji na vijiji vyote nchini usiku wa kuamkia leo walikusanyika misikitini na katika vituo vya kidini na barabarani katika marasimu ya kuadhimisha Tasu'a, siku ya tisa ya mwezi Muharram, kuelekea kwenye Siku ya Ashura ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).
Habari ID: 3482397 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA – Tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Muharram wiki iliyopita, Waislamu wa madhehebu ya Shia wameandaa majlisi na shughuli za maombolezo kukumbuka kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS) katika miji na majiji 400 nchini Niger na Nigeria.
Habari ID: 3482395 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/23
IQNA – Katika jitihada za kuimarisha usalama na kuhakikisha utulivu wakati wa siku tukufu za Tasua na Ashura katika mji mtakatifu wa Karbala, nchini Iraq, jumla ya kamera 2,000 za kisasa (smart cameras) zimewekwa kama sehemu ya mpango maalum wa kiusalama.
Habari ID: 3482392 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/23
IQNA – Maombolezo ya Muharram kwa ajili ya Imam Hussein (AS) yamefanyika karibu na Husseiniyeh ya Imam Khomeini (RA) jijini Tehran, siku ya Jumapili jioni.
Habari ID: 3482391 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/22
IQNA – Makao Makuu ya Arbaeen ya Imam Hussein (AS) nchini Irani yametangaza rasmi tarehe za kuanza kwa usajili wa waumini wanaokusudia kushiriki katika matembezi ya Arbaeen ya mwaka huu nchini Iraq.
Habari ID: 3482389 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/22
IQNA – Mtafiti kutoka Lebanon ametoa uchambuzi wa kihistoria akichunguza jinsi mila za maombolezo kwa Imam Hussein (AS) na mashahidi wa Karbala zilivyobadilika katika karne tano za kwanza za kalenda ya Hijiria, akibainisha hatua tatu tofauti kuanzia huzuni ya binafsi hadi ibada ya hadhara.
Habari ID: 3482383 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/20
IQNA – Maombolezo ya Muharram si vitendo vya huzuni tu; bali kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia kote duniani, ni uhai wa imani iliyodumu kwa karne kumi na nne, amesema mwanazuoni mmoja wa Kiislamu.
Habari ID: 3482370 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/17
IQNA – Katika kuukaribisha mwezi wa Muharram wa kalenda ya Hijria, Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) mjini Karbala, Iraq, imetangaza tarehe ya hafla ya kubadilisha bendera ya kuba la haram hiyo.
Habari ID: 3482364 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/15
IQNA – Kuta na viwanja vya makaburi au haram tukufu za Imam Hussein (AS) na Hadhrat Abbas (AS) katika mji wa Karbala, Iraq, vimepambwa kwa bendera nyeusi na alama za maombolezo huku mwezi wa Muharram wa kalenda ya Hijria ukikaribia.
Habari ID: 3482356 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/13
IQNA – Uongozi (Mfawidhi) wa Haram tukufu ya Imam Hussein (AS) umetangaza utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa muundo wa zege wa uwanja wa Imam Hassan al-Mujtaba (AS). Mradi huu utatekelezwa kwa jina la “Kutoka Arubaini hadi Arubaini” na unatarajiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa Rabi’ al-Awwal 1448 Hijria (Agosti 14, 2026).
Habari ID: 3482273 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/23
IQNA – Mutawalli wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) amesisitiza kuwa kulea na kukuza haiba au shakhsia ya Kiislamu kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu ni msingi wa kujenga jamii kamilifu na yenye fadhila.
Habari ID: 3481935 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/14
IQNA – Chuo cha elimu ya Kiislamu kwa jina la Chuo cha Imam Muhammad Baqir (AS) kimefunguliwa rasmi katika mji wa Qani, nchini Nigeria.
Habari ID: 3481926 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/12
IQNA-Tamasha la kimataifa la Chemchemi ya Shahada limefanyika kwa mara ya 18 katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq mapema wiki hii. Uzinduzi wa tamasha ulifanyika katika Haram ya Imamu Hussein (AS), na kuhudhuriwa na mwakilishi wa kiongozi mkuu wa Washia wa Iraq pamoja na ujumbe kutoka nchi takriban nchi 50.
Habari ID: 3481846 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/25
IQNA – Leo ni Ijumaa tarehe Tatu Rajab 1447 Hijria sawa na 23 Januari mwaka 2026. Siku kama ya leo miaka 1443 iliyopita, alizaliwa Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS) mjukuu mtukufu wa Mtume Muhammad (SAW).
Habari ID: 3481835 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/23