Kongamano hili litaandaliwa na idara kwa kushirikiana na kituo hicho pamoja na taasisi kadhaa za kitaaluma, vyuo vikuu, na vituo nchini Iraq.
Kaulimbiu ya tukio la kielimu la mwaka huu ni: “Ziyara ya Arubaini: Dhihirisho la Thamani za Kiroho na Maendeleo ya Kielimu.”
Malengo ya Kongamano yametajwa kuwa ni”
- Kuimarisha Mradi wa Ustaarabu: Kutoa mwangaza kuhusu umuhimu wa ustaarabu, ambao moja ya dhihirisho lake ni Ziyara ya Arubaini, na kusisitiza thamani zake za juu za kibinadamu mbele ya changamoto za kifikra.
- Kuhamasisha Utafiti: Kutoa msaada kwa tafiti zinazohusiana na Ziyara ya Arubaini katika nyanja mbalimbali.
- Kudhihirisha Jukumu la Thamani za Kibinadamu: Kuchukua mafunzo muhimu kwa ajili ya kuunda jamii bora - kulingana na mpango wa marekebisho uliiongozwa na Imam Hussein (AS).
- Kuimarisha Ushirikiano wa Kitamaduni: Kuhamasisha mazungumzo ya wazi kuhusu masuala ya kitamaduni na kijamii kwa kuheshimu maoni ya wengine.
- Uchunguzi wa Vitendo vya Mamlaka Zilizopita: Kuchunguza matendo ya serikali zilizopita (zilizokuwa zikitawala Iraq) kuhusu mjumuiko wa Ziyara ya Arubaini na mbinu walizotumia dhidi ya wafanyaziara.
- Kuunda Mazingira Sahihi ya Kielimu: Kuunda mazingira yanayohamasisha mawasiliano na uwasilishaji wa mawazo mapya ili kupata suluhisho endelevu kwa changamoto nyingi.
- Nyaraka za Bidhaa za Kifikra: Kuchapisha matokeo ya kifikra ya watafiti katika jarida maalum la kisayansi la kituo hicho.
- Kuimarisha Mshikamano wa Kidini na Kitaifa: Kuhamsha thamani za juu za kibinadamu na kugeuza Ziyara ya Arubaini kuwa tukio la ustaarabu linalokusanya pamoja makundi yote ya Kiraqi na jamii za Kiislamu na kibinadamu.
- Fursa za Utafiti kwa Watafiti: Kutoa fursa za utafiti wa shambani ili kufahamu utamaduni wa Ziyara ya Arubaini na mfumo wa thamani za kibinadamu zinazoundwa na mahujaji.
- Utafiti kuhusu Teknolojia ya Kisasa: Matumizi ya zana za kiteknolojia katika uboreshaji wa huduma za umma kwa wanaoshirikia Ziyara ya Arubaini, kama vile matumizi ya Akili Mnemba.
- Kuchunguza Tukio la Umati Mkubwa wa Washiriki wa Ziyara ya Arubaini: Kuchambua na kuangalia wingi wa watu wanaohudhuria Ziyara ya Arubaini kila mwaka na kutoa mitazamo na programu muhimu za kusimamia idadi hiyo.
Kituo kimealika wanazuoni na watafiti kuwasilisha makala zao kuhusu mada za kongamano.
Waandishi wa makala zilizochaguliwa wataalikwa kuhudhuria kongamano na kuwasilisha kazi zao huko Karbala (makazi na malazi vitatolewa na Kituo cha Karbala cha Tafiti na Utafiti).
Mwisho wa kuwasilisha makala ni Juni 15, 2025, na kongamano la kimataifa litafanyika Karbala mnamo Agosti 17-18, 2025.
3492675