IQNA

TEHRAN (IQNA)- Huku Iran ikiadhimisha wiki ya malenga mashuhuri wa Kifarsi Hafidh (Hafez au Hafiz), maonesho ya vitabu chini ya anuani ya ‘Hafez na Qur’ani’ yammefanyika katika kaburi lake ambalo ni maarufu kama Hafezieh mjini Shiraz kusini mwa Iran.

Tarehe 12 Octoba sawa na 20 Mehr Hijria Shamsiya inasadifiana na maadhimisho ya Khaja Shamsuddin Muhammad Hafidh Shirazi, mshairi na malenga mkubwa wa Kiirani. Hafidh alizaliwa mwaka 727 Hijiria Shamsia huko Shiraz moja ya miji ya kusini mwa Iran. Alikuwa mtaalamu katika tafsiri ya Qur'an, falsafa na fasihi ya Kiarabu na alipata umashuhuri kwa jina la Hafidh kutokana na kuhifadhi kwake Qur'an Tukufu kwa visomo tofauti. Mbali na elimu hizo, Khaja Shamsuddin Muhammad Hafidh, alikuwa pia mtaalamu mkubwa wa elimu ya Irfan. 

 
 
Tags: shirazi ، iran ، hafidh